NANDY AMFANYIA KITU MBAYA BRIGHT
Mwimbaji wa Bongofleva, Bright amedai kuwa Nandy kwa sasa hapokei simu zake licha ya huko nyuma kumsaidia kupitia kolabo yao, Umebadilika (2017) ambayo ilimtangaza zaidi African Princess huyo.
"Watu hawana shukrani, nilimsaidia Nandy wakati hajajulikana vizuri, tukafanya nae wimbo watu wakamjua kwa ukubwa lakini baada ya kupata mafanikio zaidi yangu hataki tena kusikia habari zangu na hata simu zangu hapokei. Umri wangu bado mdogo ipo siku nitafanikiwa"- Bright.