YANGA KUJIPIMA NA JKU
Na Tom Cruz
Kikosi cha Yanga siku ya Jumamosi kinatarajiwa kucheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar katika kipindi hiki
ambacho ligi imesimama kwa ajili ya michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko lvory Coast
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aliwaagiza viongozi wa Yanga kuhakikisha wanapata angalau mechi mbili kila wiki ili
kuhakikisha kikosi chake kinaendelea kubaki katika hali ya ushindani
Uongozi wa Yanga pia unatafuta timu nyingine kutoka nje ambayo itatoa upinzani unaoendana na mechi ambazo Yanga itakwenda kucheza pale michuano ya Afcon
2023 itakapomalizika
Gamondi amesema ni muhimu kwa vijana wake kupata mechi za kujipima nguvu ili kuona
wamefanikiwa kwa kiasi gani katika maandalizi wanayoendelea nayo
"Tumerejea mapema kwenye mazoezi kuweza kujijpanga kwa muda huu ambao upo kwa sasa, unajua tuna wachezaji wapya ambao wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, tupo nao kwenye mazoezi hivyo ni vizuri kupata michezo ya kirafiki kuangalia kikosi chetu"
"Tunalenga kuboresha timu yetu tukiwa na malengo ya kufanya vizuri kimataifa, michezo hii ya kirafiki baada ya kuongeza wachezaji itanipa picha ya nini napaswa kuongeza au
kuboresha," amesema Gamondi.