NEVER TIGERE AREJEA KWAO ZIMBABWE
Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Never Tigere Amejiunga na klabu ya Ngezi Platinum Stars ya Zimbabwe kwa Kandarasi ya mwaka mmoja nusu Akitokea klabu ya Ihefu SC ya Tanzania kwa Uhamisho Huru Baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Ihefu SC.
Tigere atakumbukwa kwa assist zake za mabao ya Ihefu dhidi ya Yanga ambapo timu hiyo ilipekeka salamu za ushindi mara mbili mfululizo huku pia akiweza kuifunga Yanga kwa mipira ya adhabu ndogo