RIYAD MAHREZ ATUNDIKA DARUGA ALGERIA
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Algeria Riyad Mahrez mwenye umri wa Miaka (32) Ametangaza rasmi Kustaafu kuitumikia timu yake ya Taifa ya Algeria baada ya kuondolewa kunako michuano ya AFCON 2023 huko Nchini Ivory Coast hatua ya makundi.
Mahrez Alianza Kuitumikia timu ya Taifa ya Algeria mwaka 2014 na mpaka anastaafu Kuitumikia Timu hiyo ya Taifa Baada ya Kuhudumu miaka (10) amecheza mechi (93) na Kufunga Magoli (31) na Kafanikiwa kushinda ubingwa AFCON Mwaka 2019 nchini Egypt.