ANGOLA WANAKWENDA ROBO FAINALI
Mabao matatu yaliyowekwa kimiwni na Delson Dala dakika ya 38 na dakika ya 42 huku lingine likiwekwa wavuni na Mabululu dakika ya 66 yametosha kabisa kuilaza Namibia mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la mataifa Afrika, AFCON nchini Ivory Coast.
Kwa ushindi huo sasa Angola watacheza na mshindi wa mechi ya baadaye kati ya Nigeria na Cameroon
Hata hivyo kipa wa Angola Neblu alionueshwa kadi nyekundu wakati Luneni Haukongo naye alionyeshwa kadi nyekundu