KIDUKU AMJIBU MWAKINYO

Vita ya maneno kati ya mabondia Twaha Kiduku na Hassan Mwakinyo imezidi kushika kasi, baada ya Kiduku kuandika ujumbe kwenye Instagram ukionekana ni ujumbe uliomlenga Mwakinyo.

Baada ya Bondia Hassan Mwakinyo kumtwanga kwa TKO bondia Elvis Ahorgah kutoka Ghana katika raundi ya Saba ya Pambano la ubingwa wa WBO Afrika.

Kufuatia ushindi huo Mwakinyo aliweka wazi kuwa ametuma salamu Morogoro kuwa yupo tayari kupigana.

“Nilikuwa nataka kutuma salamu Morogoro kwa watu ambao walikuwa wanaamini naogopa zile Piko kama mabibi harusi wa huku nilikuwa nataka kutumia hii Fursa kama mfano kuonesha kwamba dau likifikiwa ambalo lipo katika nakubaliano yangu mimi na timu yangu pambano litapigwa hata la kirafiki ili tuone nani ni nani.” amesema Mwakinyo.

Nae Twaha Kiduku bondia kutoka Morogoro kupitia mtandao wa Instagram kwenye ukurasa wake ameandika . ‘’Mwenye hasira nyingi,ana hekima chache.”

Twaha Kiduku

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA