CISSE KOCHA BORA HATUA YA MAKUNDI AFCON
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Senegal Aliou Cissé amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON 2023.
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Senegal Lamine Camara amechaguliwa kuwa Mchezaji bora Chipukizi wa Michuano ya AFCON 2023 hatua ya makundi.
Na Golikipa wa Timu ya Taifa ya Equatorial Guinea Jesús Owono amechaguliwa kuwa Golikipa Bora wa Michuano ya AFCON 2023 hatua ya makundi.