MZIZE APIGA HAT TRICK, YANGA IKIICHAPA HAUSING FC 5-1
Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup, maarufu ASFC au kombe la FA, Yanga SC usiku huu imeichapa Housing FC ya mkoani Njombe mabao 5-1 katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Yanga walitangulia kupata bao kupitia kwa Jonas Mkude kynako dakika ya 19 kabla ya Skudu Makulubela kuandika la pili dakika ya 25.
Lakini Clement Mzize alifunga mabao yote matatu kunako dakika ya 27, 33 na 57, Tony Jailos aliifungia Housing bao LA kufuta machozi dakika ya 70, kesho Simba wataumana na Tembo ya Tabora