WINGA SENEGAL AISHUTUMU CAF
Winga wa timu ya Taifa ya Senegal, Krepin Diatta ameibua hoja ya rushwa akiwatuhumu waandaaji wa mashindano ya AFCON Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwadhulumu haki yao kwenye mchezo wa hatua ya (16) Bora dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo Ivory Coast na kuwapa upendeleo wenyeji.
“Mmetudhulumu, mashindano yamejaa rushwa bakini na Kombe lenu” alisema Diatta, Hii ni baada ya Ivory Coast kupata penati dakika za mwishoni ,penati iliyoamuliwa na VAR, Hata hivyo mchezaji huyo anaweza kukutana na adhabu kutoka CAF kwa kuwatuhumu kuendesha mashindano kwa rushwa.