Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2023

ISMAIL MHESA AITOSA MASHUJAA

Picha
Winga wa Kitanzania Ismail Aidan Mhesa ameachana na klabu ya Mashujaa FC ya Kigoma Baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Ismail alijiunga na Mashujaa FC mwanzoni mwa msimu huu wakati wa dirisha kubwa la Usajili na Sasa mambo hayajaenda Vizuri hivyo ameachana na klabu hiyo. Mhesa kwasasa yuko katika mazungumzo na klabu ya Mtibwa Sugar FC ambayo alicheza kabla ya kwenda kujiunga na Mashujaa FC.

MAYELE ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUUA MWANAJESHI

Picha
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na polisi wa mkoa wa Ruvuma wamemkamata Rakeshi Kato (24) maarufu kama Mayele kwa mauaji ya Afisa wa JWTZ aliyemchoma kwa kitu chenye ncha kali kilichopelekea kifo chake maeneo ya Kawe mnamo Oktoba 25, 2023. Taarifa hiyo imetolewa hii leo Desemba 31, 2023, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambapo amesema kijana huyo baada ya kutekeleza tukio hilo amekuwa akikimbilia katika mikoa mbalimbali ambapo kwa jitihada za kiitelejensia za jeshi hilo lilimkamata na alikiri kufanya tukio hilo.

YANGA YAENDELEZA 5 HADI KOMBE LA MAPINDUZI

Picha
Yanga SC imewapa zawadi ya kuaga mwaka wa 2023 kwa kuendeleza vipigo vyake vya mabao matano, hasa baada ya usiku huu kuifumua Jamhuri ya Pemba mabao 5-0 katika uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar. Ushindi huo mkubwa wa kombe la Mapinduzi umeifanya Yanga kuweka hai matumaini yake ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo. Mabao ya Yanga yamefungwa na Crispin Ngushi aliyefunga mawili, Kibwana Shomari, Walid Mzize na Skudu Makulubela

OKRAH NI WA YANGA

Picha
Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC imemtambulisha mchezaji wake mpya Augustine Okrah atakayeitumikia klabu hiyo kuanzia sasa hadi 2026 mkataba wake utakapomalizika. Okrah amejiunga na Yanga akitokea klabu ya Bemchem ya Ghana aliyojiunga nayo msimu uliopita akitokea Simba SC ambao ni mahasimu wa Yanga. Usajili wa Okrah unaweza kuwaliza watani zao kwani mchezaji aliondoka klabuni hapo akidaiwa ni mgonjwa na pia ni mtovu wa nidhamu, jambo ambalo si kweli

MIQUISSONE AIGOMEA SIMBA

Picha
Klabu ya Simba kwenye dirisha hili la usajili inahitaji kufanya maboresho kwa kufanya maingizo ya nyota wapya wa kigeni watakaokuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chao. Ili maingizo hayo yafanyike ni lazima waachane na baadhi ya nyota wa kigeni kwani kikanuni tayari wametosha.Sheria za Ligi kuu zinaitaka klabu moja kuwa na wachezaji [12] pekee wa kigeni. Nyota ambao walitakiwa kupunguzwa ni pamoja na Luis Miqquisone ambaye hajawa na makali tangu alipojiunga na kikosi hicho.Simba ilipanga kumtoa kwa mkopo ili akaimarishe kiwango chake lakini nyota huyo amegoma. Luis amewaambia wadosi kuwa anataka kuendelea kusalia kikosini hapo na huenda akarejesha kiwango chake kama awali.

SIMBA NAYO YASAJILI MCOLOMBIA HATARI

Picha
Klabu ya Simba Imekamilisha Usajili wa Winga Mauricio Cortes Nunez Mwenye Umri Wa Miaka 26 Raia Wa Colombia. Winga Huyo Kutoka Klabu ya Commerciantes ya Colombia Atawasili Jumanne Dar es salaam Tanzania Kwaajili ya Kukamilisha Taratiibu za Kusaini Mkataba Wa Miaka Miwili Msimbazi. Winga Huyo Ambae Kwenye Michezo 8 ya Mwisho Ameweka Kambani Bao 2 na kutengeneza 3 Anatarajiwa Kuvuna Mshahara Wa Tsh Milioni 44 Kwa Mwezi Huku Dau lake la Usajili Likitajwa kuwa ni Tsh mil 586.

AZAM YASHINDA KWA MBINDE

Picha
Goli pekee lililofungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza na mshambuliaji bonge wa Azam FC Alassane Diao liliiwezesha matajiri hao wa Chamazi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar usiku wa leo katika michuano ya kombe la Mapinduzi. Hiyo ni mechi ya pili kwa Azam ambao katika mchezo wao kwanza walilazimishwa sare isiyo na bao dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Mlandege

CHAMA, INONGA NA MUSONDA KUCHEZA AFCON

Picha
Clatous Chama amekuwa mchezaji wa pili kutoka Simba SC Tanzania baada ya Enock Inonga Baka kuthibitishwa kushiriki AFCON 2023 itakayofanyika Cote De Voire kuanzia January hii akiwa na Chipolopolo (Zambia . Mpaka sasa ni wachezaji watatu tu kutoka Ligi Kuu bara ya NBC waliothibitishwa kwenda AFCON, wachezaji hao ni Hennock Inonga, Clatous Chama na Kennedy Musonda

MWINYI KUTILIA MKAZO UJENZI WA VIWANJA VYA MICHEZO

Picha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Awamu ya nane inatilia mkazo ujenzi wa viwanja vya michezo mbalimbali ili kutanua wigo wa ajira kutokana na michezo pamoja na kuibua vipaji vya vijana. Amesema azma ya Serikali ni kuendeleza michezo katika nyanja zote inatimia kwa kuweka miundombinu ya kisasa iliyobora na imara. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoufungua Viwanja vya Michezo Matumbaku Sports Complex uliopo Shehia ya Miembeni, Mkoa wa Mjini Magharibi katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe: 30 Disemba 2023. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewatoa hofu wananchi wa Malindi kuwa dhamira ya ujenzi wa viwanja hivi ni kuwa mbadala maeneo yaliyofanyiwa uwekezaji. Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewataka vijana watumie fursa za kuwepo kwa viwanja vipya vya kisasa kwa kuonyesha vipaji vyao ili waweze kutengeneza ajira ndani ya nchi na nje. Pia amesema michezo ikitumika vizuri itakuwa ni fursa ya kuitangaza Zanzibar ...

MBADALA WA LOMALISA YANGA HUYU HAPA

Picha
Na Elius John Yanga imedhamiria kuboresha kikosi chake kila mahali ambapo tayari imetua upya nchini DR Congo, kwa ajili ya kukamilosha dili la kumpata beki wa kushoto, Kasapu lbrahim Abduol ambaye anakipiga Maniema Union ya DR Congo. Abduol anakuja kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu na Hadi Sasa hajasaini mkataba mpya licha ya kushawishiwa afanye hivyo

ZAHERA KOCHA MKUU NAMUNGO

Picha
Klabu ya Namungo imemtangaza rasmi Mwinyi Zahera raia wa DR Congo kuwa Kocha Mkuu wao Mpya akichukua nafasi ya Denis Kitambi ambaye amejiunga na Geita Gold. Zahera ambaye amewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio ikimaliza ligi kwenye nafasi ya pili nyuma ya Simba pia aliifundisha Coastal Union ya Tanga ambao walimfuta kazi hivi karibuni Mwinyi Zahera kocha mpya Namungo FC

MOSES PHIRI ATIMKIA APR

Picha
Klabu ya APR ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Simba ili kuipata saini ya mshambuliaji raia wa Zambia, Moses Phiri kwa mkataba wa mkopo katika dirisha hili dogo la uhamisho la msimu huu. Kwa mujibu wa Abdelhak Benchikha ameuambia Uongozi wa Simba kuwa anahitaji kufanya kazi na wachezaji wenye umri mdogo huku Moses Phiri hayupo kwenye mipango yake ya kuitengeneza timu bora. Taarifa za kuaminika ni kuwa Moses Phiri amekubali kujiunga na APR baada ya klabu hiyo kuiomba Simba kumtoa kwa mkopo Moses Phiri na Simba haitarajii kumtoa mchezaji huyo kwenye timu iliyotwaa kombe la Ligi Kuu msimu uliopita.

CHAMA KUTAMBULISHWA YANGA

Picha
Muda wowote klabu ya Yanga itatangaza kumsainisha kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Mzambia Clatous Chama. Chama amesimamishwa kwa muda usiojulikana na waajili wake Simba wakidai ni mtovu wa nidhamu sambamba na kiungo Nassoro Kapama. Lakini vyanzo vyetu vya habari vinasema tayari Yanga wameshazama ndani na kuzungumza na Chama ambaye mkataba wake na Simba umesalia miezi 6 hivyo ifikapo dirisha kubwa la usajili atajiunga na Yanga

NYOTA MONASTIR YA TUNISIA KUTUA SIMBA

Picha
Simba imepanga kusajili wachezaji wasiopungua 5 katika usajili wa dirisha dogo. Ladack Chasambi tayari ni Mnyama, kwasasa inataka kupindua dili la Edwin Balua kujiunga na Sarpsborg 08 ya Norway Mazungumzo yamefikia hatua nzuri. Kiungo Mkabaji Babacar Sarr (26) wekundu wa Msimbazi akitokea Monastir Dili lake limefikia hatua nzuri, kama kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, basi wiki hii anatarajia kutua Tanzania kwaajili ya kukamilisha usajili huo. Valentino Mashaka kutoka Geita Gold FC anatajwa kwenye mazungumzo ya mabosi wa Simba but Nothing Serious, hadi sasa hajapata ofa rasmi. Pia, Kwa mujibu wa @kiddy87_jr : Klabu ya Simba imekamilisha deal la mchezaji raia wa Colombia Mauricio Cortés, ambaye Viongozi walikuwa kwenye mazungumzo na wakala wake Ceballos na makubaliano yamekalika. Mchezaj huyo atajiunga na Simba mpaka mwaka 2025, Mkataba wa Miaka miwili .

AZAM FC YAMTOSA DJUMA SHABANI

Picha
Inasemekana kwamba Azam FC haina mpango wa kunsajili beki wa zamani waYanga SC Djuma Shabani. Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa klabu hiyo Hasheem Ibwe ambapo amedai hawana mpango wa kumsajili isipokuwa alikuwa anafanya mazoezi tu ili kulinda kiwango chake. "Unajua Azam FC ni miongoni mwa timu ambayo ina mahusiano na klabu nyingi za hapa nyumbani nje lakini pia wachezaji mmoja mmoja kwasababu ukimtoa Shabani Djuma ambae anatajwa yupo Hassan Dilunga ambae wakati anapata majeraha makubwa alikuwa na Simba SC, na kupona kwake alipona Azam FC, ambapo alikuwa anafanya mazoezi na sisi, Shabani Djuma hakuwa mchezaji wa Azam FC ni mtu ambae alikuwa akifanya mazoezi akilinda kiwango chake." - amesema Afisa Habari wa Azam FC, hasheem ibwe

MIQUISSONE KUONDOKA SIMBA

Picha
LUIS KUONDOKA SIMBA SC Inaelezwa Simba SC ipo kwenye mpango wa kuachana na baadhi ya nyota wao wa Kigeni na wengine kuwaondoa kwa mkopo kwenda kuboresha viwango vyao akiwano Winga Luis Miquissone ambae inaelezwa mnyama anapanga kumtoa kwa mkopo ili kupisha nyota wengine kwenye nafasi yake. Nyota huyo Luis Miquissone amewagomea viongozi wa Simba SC kuondoka kwa mkopo akihitaji kupewa muda zaidi wa kupambana akiamini ana uwezo wa kurejesha kiwango chake kama ambavyo kilikuwa wakati anaondoka kujiunga na Al Ahly ya Misri. Simba SC inapaswa kuwaondoa baadhi ya nyota wake wa Kigeni ambapo kikanuni imefikisha idadi ya wachezaji 12 wanaotakiwa kikanuni ili kuwapisha wengine kwenye dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kumpa nafasi Abdelhak Benchikha kukiboresha kikosi chake.

AZAM FC YAVUTA KIFAA CHA COLOMBIA

Picha
Klabu ya Azam FC imethibitisha kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa klabu ya Cortulu'a Franklin Navarro raia wa Colombia,. Navarro mwenye miaka 23 mwaka huu akicheza Ligi daraja la pili nchini Colombia amefunga jumla ya bao moja na kutoa assist mbili katika mechi 14 Hawa ndoo matajili Tanzania nzima

RDWIN BALUA AITOSA YANGA

Picha
Kuna uwezekano mkubwa sana kiungo wa Tanzania Prisons Edwin Barua akajiunga Sarpsborg 08FF ya Norway. Ninachojua Young Africans walionyesha nia ya kuhitaji huduma yake but nothing was serious SimbaSimba SC Tanzaniaingia kwenye mazungumzo na Edwin Barua, na huenda dili la kwenda Norway likafa na Mwamba huyu akajiunga na Club ya Simba.

OKRAH ASAINI YANGA

Picha
Klabu ya Yanga SC imemalizana na winga wa zamani wa Simba SC Augustine Okrah kwa kandarasi ya mwaka mmoja na nusu. Imefahamika kwamba Yanga imeridhishwa na kiwango cha Okrah ambaye msimu uliopita aliachwa na Simba kwa sababu ya utovu wa nidhamu pamoja na kushuka kiwango. Lakini Rais wa Yanga Injinia Hersi alipoenda Ghana wakati Yanga ikienda kucheza na Medeama alipiga stori na Okrah na kugundua kwamba Simba ilimuacha kimizengwe hivyo akaamua kumchukua. Mpaka sasa Okrah anayecheza winga amefunga mabao 9, assist mbili katika mechi 14 alizocheza kwenye klabu ya Benchima

HONGERA TABIA BATAMWANYA KWA KUSHINDA TUZO

Picha
Na Prince Hoza HONGERA sana tena sana mwanadada Tabia Batamwanya kwa kushinda tuzo ya mwimbaji bora wa muziki wa dansi ilitolewa hivi karibuni, haikuwa rahisi kwa mwanadada huyo kubeba tuzo hiyo kwani ameipigania kwa muda mrefu sana.  Batamwanya ni msanii wa siku nyingi lakini jina lake limeanza kufahamika hivi karibuni kutokana na kuvuma kwa wimbo wake wa "Narudi nyumbani" aliomshirikisha mwanamuziki wa bongofleva Uncle Some.  Batamwanya alianza kujulikana tangu mwaka 2006 pale alipojikita kwenye sanaa ya ulimbwende, msanii huyo aliibuka mshindi wa Miss Singida na kufanikiwa kushiriki mashindano ya Miss Tanzania.  Ikumbukwe Batamwanya alishiriki sambamba na Wema Sepetu ambaye aliibuka mshindi na kuwakilisha Tanzania kwenye Miss World, safari ya Batamwanya kwenye urembo nadhani iliishia hapo na alijikita kwenye muziki wa dansi.  Batamwanya ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa muziki wa dansi nchini Jumbe Batamwanya ambaye alihudumu katika bendi ya Bima Lee Orchestra ambapo al...

KIBU ANATAKIWA WYDAD

Picha
Tetesi kutoka kwenye chanzo cha kuaminika zinasema Simba SC imopokea Barua kutoka klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco wakihitaji saini ya nyota wa kimataifa wa Tanzania, Kibu Dennis Kutokana na ubora na kiwango alichokionesha katika mechi walizokutana Kibu D imewavutia zaidi waarabu hao na kulazimika kutuma maomba ya kuhitaji huduma yake. Hata hivyo hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na pande zote mbili.

HUU NDIO UWANJA WA AMAAN STADIUM

Picha
Hivi ndivyo ulivyo uwanja mpya wa Amaan hasa baada ya leo tarehe 27/12/2023 kuzinduliwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

MIL 40 KUMSHUSHA MODIBA MSIMBAZI

Picha
Aubrey Modiba ambaye ana husishwa kuwindwa na timu ya Simba SC kwa mwezi anakunja milion 39 akiwa pale Mamelodi Sundowns. Nyota huyu ambaye kwa sasa hucheza nafasi ya kiungo wa kati Soccer Laduma wameripoti anasakwa na Wekundu wa Msimbazi. Ili Simba SC wamshawishi Modiba lazima wapande Dau kubwa zaidi na bonasi za kutosha Kwa sababu Mamelodi Sundowns mshahara wake ni Randi 290000 kwe mwezi hivyo Ukigeuza Kwa Shilingi hapo inakuwa Milion 39 ....Pointi kadhaa nyota huyu anachukua .

TANZANIA BARA, ZANZIBAR HAKUNA MBABE

Picha
Time za taifa za Tanzania bara, Kilimanjaro Stars na Zanzibar, Zanzibar Heroes zimetoka sare isiyo na mabao usiku huu katika uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar. Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa ni maalum kwa ufunguzi wauwanja mpya wa Amaan ambao umekamikika baada ya kufanyiwa matengenezo mapya chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi

PACOME AIMWAGIA SIFA YANGA

Picha
Baada ya kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua kujumishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake la Ivory Coast kwanza ameishukuru Yanga kwa kumbeba. Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha Tembo kitakachokwenda kushiriki fainali hizo zinazofanyika hapohapo nchini kwao. Akizungumza Pacome alisema ingawa amewahi kuzitumikia timu za taifa kwa vijana za taifa hilo lakini akasema haikuwa rahisi kuitwa timu ya wakubwa. “Nilikuwa mchezaji bora wa ligi msimu uliopita kule Ivory Coast lakini sikupata bahati kama hii, ndani ya muda mfupi nikiwa hapa Yanga naitwa timu ya taifa hii ni bahati.,” alisema Pacome.

SIMBA KUIBOMOA JKU

Picha
Klabu ya Simba ipo kwenye rada ya kuimarisha safu yake ya ulinzi na wanatajwa kuanza kumuwinda beki wa JKU ya Zanzibar Mcameroon Jean Jospin Engola. Beki huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2 na uwezo mkubwa wa kujilinda na mipira iliyokufa, aliwahi kucheza Lagalax Marekani Na Coton Spots ya Cameroun.

SIMBA NA YANGA KUVUNA BIL 153 WAKISHIRIKI KOMBE LA DUNIA

Picha
Unaambiwa endapo Klabu mojawapo kati ya Simba au Yanga ikifanikiwa kufuzu kucheza kombe la Dunia la klabu kwa mwaka 2025 basi itakabidhiwa kitita cha Euro Millioni 50+ ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 153+ kwaajili ya kufanya maandalizi binafsi. Pesa hiyo huongezeka kadiri mshiriki anapozidi kusogea katika hatua za mbele zaidi kama robo, nusu na fainali ya kombe hilo huku bingwa akikabidhiwa Euro Milioni 100 sawa na shilingi Bilioni za kitanzania 276 na Milioni 300+. Njia pekee ya Simba na Yanga kushiriki kombe hili kwa mwaka 2025 ni kuhakikisha zinalitwaa Kombe la #CAFCL msimu huu lasivyo hawatokidhi vigezo vya kupata nafasi hii.

SHIZA KICHUYA KUIBUKIA JKT TANZANIA

Picha
Winga wa Namungo FC, Shiza Kichuya kuna asilimia kubwa pindi litakapofungwa dirisha dogo la usajili linaloendelea kwa sasa, akaibukia JKT Tanzania, inayonolewa na kocha Malale Hamsini. . Mambo Uwanjani imepata taarifa za ndani kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa timu ya JKT Tanzania kwamba kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kinaenda sawa na muda wowote anaweza akasaini. Japokuwa haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Kichuya alibakiza na Namungo, lakini inaelezwa taratibu zote zinafuatwa ili kuhakikisha wanainasa saini yake.

MSUVA AMALIZANA NA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr Mshambuliaji Simon Msuva anatajwa kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC na muda wpwote kuanzia sasa anaweza kutambulishwa. Msuva ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni alivunjiwa mkataba wake na timu ya JS Kybalie ya Algeria. Msuva pia amewahi kuichezea Wydad Casablanca ya Morocco na pia aliwahi kucheza Saudi Arabia

ZAI MIDEKO AZAMA KWENYE PENZI LA BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA

Picha
Na Shafii Matuwa STAA wa muziki wa singeli ambaye pia ni muigizaji Zai Mideko amejikuta akizama kwenye penzi la bondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini Nurdin Mijibwa. Mwandishi wa habari hizi amemkuta Mideko mitaa fulani akiwa na Manama sum who huyo anayepigania uzito wa Feadher, Mideko na Mijibwa walikuwa wamekaa kwenye kona moja huku wakishikana na jinsi walivyo kwa vyovyote ni wapenzi.  Hata hivyo mwanahabari wetu aliamua kuwasogelea kwa ukaribu na kwakuwa Mijibwa ni staa wa ngumi na Mideko ni staa wa muziki akaamua kuzungumza nao, Mijibwa akuwa tayari kuzungumza lolote isipokuwa Mideko alisikika akisema aachwe na mpenzi wake na ipo siku ataanika uhusiano wake na Mijibwa.  "Ni kweli Mijibwa nampenda sana lakini itafika siku nitaanika mahusiano yangu na Mijibwa, ila kwasasa siambiwi wala kusikia lolote kwa bondia huyu ndio usingizi wangu", alisema Mideko  

SIMBA YARUDI TENA KWA YAHYA MBEGU

Picha
Klabu ya Simba imeanza mazungumzo na Menejiment ya mlinzi wa kushoto wa Singida Fountain Gate, Yahya Mbegu ili kuipata saini ya mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili. Yahya Mbegu bado anahitajika na Klabu ya Simba ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kushoto ambalo hivi sasa linahudumiwa na mlinzi wa kushoto Mo Hussein.

CHE MALONE ATEMWA, ATEBA AJUMUHISHWA CAMEROON

Picha
Mshambuliaji hatari wa Dynamo Douala, Leonel Ateba amejumuishwa kwenye kikosi cha Wachezaji 55 wa Cameroon kitakachoelekea nchini Ivory Coast kwa ajili ya michuano ya AFCON 2023. Huku mlinzi Che Malone aliyetajwa kwenye kikosi cha awali ameondolewa kwenye kikosi hicho cha Kocha Mkuu Rigobert Song wa Cameroon.

USHAURI WA ALLY KAMWE KWA AHMED ALLY

Picha
Shida ni kwamba  Timu inaposhinda Msemaji unajimilikisha ushindi huo. Unatamba nao na kujipa kila aina ya majina kuonyesha kwamba Wewe ni KILA KITU kwenye Ushindi. Lakini timu inapopata matokeo mabaya, Unajitenga nayo. Unaanza kutupa lawama hadharani kwa wachezaji kuwa hawana Ubora na Uchu wa kuipa Timu mafanikio.. Huku ni KUKOSA HESHIMA. Ni Ubinafsi na unaonyesha ni kwa kiasi gani Msemaji upo kwa ajili ya kulijenga jina lako na sio kuijenga Taasisi yako. Na hii ni mbaya pindi Interest binafsi zinapotangulia kuliko Interest za Taasisi. Jambo moja ambalo inatupasa tuelewe, Nyakati nzuri na mbaya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mchezaji anayekwenda uwanjani ili apoteze mchezo. Kuwazodoa na kuwasema hadharani wachezaji wako ni kutaka kuwachonganisha na mashabiki. Ni ishara pia ya kutoheshimu kazi yao. Na hata inapobidi, wachezaji wakatakiwa kusemwa, mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Benchi la Ufundi, Sio msemaji wa Timu. Makocha wamekaa Darasani na wakafundishwa jinsi ya kuishi na kuwaelekeza wa...

STRAIKA WA RS BERKANE, YANGA ATUA COASTAL UNION

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Yanga SC, RS Berkane na Timu ya Taifa ya Burundi Fiston Abdulrazaq amesajiliwa na klabu ya Coastal Union ya Tanzania . Abdulrazak aliwahi kucheza Yanga lakini hakuweza kufanya maajabu yoyote chakushangaza RS Berkane ya Morocco ikanasa saini yake hats hivyo imeshindwa kudumu naye na Coastal Union inajaribu bahati yake kuwa naye  

KILIMANJARO STARS WAIFUATA ZANZIBAR HEROES

Picha
Timu ya taifa ya Tanzania bars, Kilimanjaro Stars imeanza safari ya kuelekea Zanzibar ambapo itaenda kucheza na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes mchezo wa kirafiki wa kudumuhisha muungano. (Pichani) Wachezaji wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakiwa Bandarini, Dar es Salaam kwa safari ya Zanzibar kucheza mchezo maalumu wa kirafiki kufungua uwanja w Amaan, mchezo utakaochezwa Desemba 27, 2023.

BUMBULI AMTETEA CHAMA

Picha
“Baada ya Chama kusimamishwa na uongozi wa Simbasc kwa sababu ya Utovu wa nidhamu watu mbali mbali wamekua na Mtazamo na maono tofauti tofauti kupitia Ukurasa wa aliekuwa Afsa Habari na Mawasiliano wa yangasc Hassan Bumbuli ameandika haya” Clatous Chota Chama, Triple C a.k.a Mwamba wa Lusaka. Hata iweje, umefanya kazi kubwa katika soka la Tanzania na umeleta ufahamu wa ajabu kwenye soka letu. Kama shabiki wa soka ninaheshimu na nitaendelea kuenzi ulichofanya. Ninakupa heshima yangu kamili.

SIMBA YABISHA HODI KOMBE LA DUNIA

Picha
Klabu ya Simba SC ya Tanzania ipo kwenye orodha ya Klabu zinazowania kufuzu Kombe la Dunia la Klabu (FIFA Club World Cup 2025).

MWAMNYETO KUTIMKA YANGA

Picha
Kwa muujibu wa Wasaf Fm, Nahodha wa kikosi cha Yanga Sc, Bakari Mwamnyeto huenda akatimka ndani ya kikosi hicho cha wananchi mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa Mwamnyeto na Yanga utafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa 2023/24 na taarifa zinaeleza kuwa zipo timu mbalimbali kutoka Morocco na Algeria zimeanza kuwinda saini ya nyota huyo. Hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Yanga na Mwamnyeto ya kutaka kumuongezea mkataba beki huyo ili aendelee kuwatumikia wananchi