SHIZA KICHUYA KUIBUKIA JKT TANZANIA
Winga wa Namungo FC, Shiza Kichuya kuna asilimia kubwa pindi litakapofungwa dirisha dogo la usajili linaloendelea kwa sasa, akaibukia JKT Tanzania, inayonolewa na kocha Malale Hamsini.
.
Mambo Uwanjani imepata taarifa za ndani kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa timu ya JKT Tanzania kwamba kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kinaenda sawa na muda wowote anaweza akasaini.
Japokuwa haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Kichuya alibakiza na Namungo, lakini inaelezwa taratibu zote zinafuatwa ili kuhakikisha wanainasa saini yake.