MIQUISSONE KUONDOKA SIMBA

LUIS KUONDOKA SIMBA SC

Inaelezwa Simba SC ipo kwenye mpango wa kuachana na baadhi ya nyota wao wa Kigeni na wengine kuwaondoa kwa mkopo kwenda kuboresha viwango vyao akiwano Winga Luis Miquissone ambae inaelezwa mnyama anapanga kumtoa kwa mkopo ili kupisha nyota wengine kwenye nafasi yake.

Nyota huyo Luis Miquissone amewagomea viongozi wa Simba SC kuondoka kwa mkopo akihitaji kupewa muda zaidi wa kupambana akiamini ana uwezo wa kurejesha kiwango chake kama ambavyo kilikuwa wakati anaondoka kujiunga na Al Ahly ya Misri.

Simba SC inapaswa kuwaondoa baadhi ya nyota wake wa Kigeni ambapo kikanuni imefikisha idadi ya wachezaji 12 wanaotakiwa kikanuni ili kuwapisha wengine kwenye dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kumpa nafasi Abdelhak Benchikha kukiboresha kikosi chake.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA