CHAMA KUTAMBULISHWA YANGA
Muda wowote klabu ya Yanga itatangaza kumsainisha kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Mzambia Clatous Chama.
Chama amesimamishwa kwa muda usiojulikana na waajili wake Simba wakidai ni mtovu wa nidhamu sambamba na kiungo Nassoro Kapama.
Lakini vyanzo vyetu vya habari vinasema tayari Yanga wameshazama ndani na kuzungumza na Chama ambaye mkataba wake na Simba umesalia miezi 6 hivyo ifikapo dirisha kubwa la usajili atajiunga na Yanga