AZAM FC YAMTOSA DJUMA SHABANI

Inasemekana kwamba Azam FC haina mpango wa kunsajili beki wa zamani waYanga SC Djuma Shabani.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa klabu hiyo Hasheem Ibwe ambapo amedai hawana mpango wa kumsajili isipokuwa alikuwa anafanya mazoezi tu ili kulinda kiwango chake.

"Unajua Azam FC ni miongoni mwa timu ambayo ina mahusiano na klabu nyingi za hapa nyumbani nje lakini pia wachezaji mmoja mmoja kwasababu ukimtoa Shabani Djuma ambae anatajwa yupo Hassan Dilunga ambae wakati anapata majeraha makubwa alikuwa na Simba SC, na kupona kwake alipona Azam FC, ambapo alikuwa anafanya mazoezi na sisi, Shabani Djuma hakuwa mchezaji wa Azam FC ni mtu ambae alikuwa akifanya mazoezi akilinda kiwango chake."

- amesema Afisa Habari wa Azam FC, hasheem ibwe


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA