SIMBA NAYO YASAJILI MCOLOMBIA HATARI
Klabu ya Simba Imekamilisha Usajili wa Winga Mauricio Cortes Nunez Mwenye Umri Wa Miaka 26 Raia Wa Colombia. Winga Huyo Kutoka Klabu ya Commerciantes ya Colombia Atawasili Jumanne Dar es salaam Tanzania Kwaajili ya Kukamilisha Taratiibu za Kusaini Mkataba Wa Miaka Miwili Msimbazi.
Winga Huyo Ambae Kwenye Michezo 8 ya Mwisho Ameweka Kambani Bao 2 na kutengeneza 3 Anatarajiwa Kuvuna Mshahara Wa Tsh Milioni 44 Kwa Mwezi Huku Dau lake la Usajili Likitajwa kuwa ni Tsh mil 586.