ZAI MIDEKO AZAMA KWENYE PENZI LA BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA
Na Shafii Matuwa
STAA wa muziki wa singeli ambaye pia ni muigizaji Zai Mideko amejikuta akizama kwenye penzi la bondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini Nurdin Mijibwa.
Mwandishi wa habari hizi amemkuta Mideko mitaa fulani akiwa na Manama sum who huyo anayepigania uzito wa Feadher, Mideko na Mijibwa walikuwa wamekaa kwenye kona moja huku wakishikana na jinsi walivyo kwa vyovyote ni wapenzi.
Hata hivyo mwanahabari wetu aliamua kuwasogelea kwa ukaribu na kwakuwa Mijibwa ni staa wa ngumi na Mideko ni staa wa muziki akaamua kuzungumza nao, Mijibwa akuwa tayari kuzungumza lolote isipokuwa Mideko alisikika akisema aachwe na mpenzi wake na ipo siku ataanika uhusiano wake na Mijibwa.
"Ni kweli Mijibwa nampenda sana lakini itafika siku nitaanika mahusiano yangu na Mijibwa, ila kwasasa siambiwi wala kusikia lolote kwa bondia huyu ndio usingizi wangu", alisema Mideko