ZAHERA KOCHA MKUU NAMUNGO
Klabu ya Namungo imemtangaza rasmi Mwinyi Zahera raia wa DR Congo kuwa Kocha Mkuu wao Mpya akichukua nafasi ya Denis Kitambi ambaye amejiunga na Geita Gold.
Zahera ambaye amewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio ikimaliza ligi kwenye nafasi ya pili nyuma ya Simba pia aliifundisha Coastal Union ya Tanga ambao walimfuta kazi hivi karibuni