MWAMNYETO KUTIMKA YANGA
Kwa muujibu wa Wasaf Fm, Nahodha wa kikosi cha Yanga Sc, Bakari Mwamnyeto huenda akatimka ndani ya kikosi hicho cha wananchi mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa Mwamnyeto na Yanga utafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa 2023/24 na taarifa zinaeleza kuwa zipo timu mbalimbali kutoka Morocco na Algeria zimeanza kuwinda saini ya nyota huyo.
Hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Yanga na Mwamnyeto ya kutaka kumuongezea mkataba beki huyo ili aendelee kuwatumikia wananchi