MAYELE ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUUA MWANAJESHI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na polisi wa mkoa wa Ruvuma wamemkamata Rakeshi Kato (24) maarufu kama Mayele kwa mauaji ya Afisa wa JWTZ aliyemchoma kwa kitu chenye ncha kali kilichopelekea kifo chake maeneo ya Kawe mnamo Oktoba 25, 2023.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo Desemba 31, 2023, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambapo amesema kijana huyo baada ya kutekeleza tukio hilo amekuwa akikimbilia katika mikoa mbalimbali ambapo kwa jitihada za kiitelejensia za jeshi hilo lilimkamata na alikiri kufanya tukio hilo.