MIQUISSONE AIGOMEA SIMBA

Klabu ya Simba kwenye dirisha hili la usajili inahitaji kufanya maboresho kwa kufanya maingizo ya nyota wapya wa kigeni watakaokuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ili maingizo hayo yafanyike ni lazima waachane na baadhi ya nyota wa kigeni kwani kikanuni tayari wametosha.Sheria za Ligi kuu zinaitaka klabu moja kuwa na wachezaji [12] pekee wa kigeni.

Nyota ambao walitakiwa kupunguzwa ni pamoja na Luis Miqquisone ambaye hajawa na makali tangu alipojiunga na kikosi hicho.Simba ilipanga kumtoa kwa mkopo ili akaimarishe kiwango chake lakini nyota huyo amegoma.

Luis amewaambia wadosi kuwa anataka kuendelea kusalia kikosini hapo na huenda akarejesha kiwango chake kama awali.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA