KIBU ANATAKIWA WYDAD
Tetesi kutoka kwenye chanzo cha kuaminika zinasema Simba SC imopokea Barua kutoka klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco wakihitaji saini ya nyota wa kimataifa wa Tanzania, Kibu Dennis
Kutokana na ubora na kiwango alichokionesha katika mechi walizokutana Kibu D imewavutia zaidi waarabu hao na kulazimika kutuma maomba ya kuhitaji huduma yake.
Hata hivyo hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na pande zote mbili.