PACOME AIMWAGIA SIFA YANGA
Baada ya kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua kujumishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake la Ivory Coast kwanza ameishukuru Yanga kwa kumbeba.
Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha Tembo kitakachokwenda kushiriki fainali hizo zinazofanyika hapohapo nchini kwao. Akizungumza Pacome alisema ingawa amewahi kuzitumikia timu za taifa kwa vijana za taifa hilo lakini akasema haikuwa rahisi kuitwa timu ya wakubwa.
“Nilikuwa mchezaji bora wa ligi msimu uliopita kule Ivory Coast lakini sikupata bahati kama hii, ndani ya muda mfupi nikiwa hapa Yanga naitwa timu ya taifa hii ni bahati.,” alisema Pacome.