OKRAH ASAINI YANGA
Klabu ya Yanga SC imemalizana na winga wa zamani wa Simba SC Augustine Okrah kwa kandarasi ya mwaka mmoja na nusu.
Imefahamika kwamba Yanga imeridhishwa na kiwango cha Okrah ambaye msimu uliopita aliachwa na Simba kwa sababu ya utovu wa nidhamu pamoja na kushuka kiwango.
Lakini Rais wa Yanga Injinia Hersi alipoenda Ghana wakati Yanga ikienda kucheza na Medeama alipiga stori na Okrah na kugundua kwamba Simba ilimuacha kimizengwe hivyo akaamua kumchukua.
Mpaka sasa Okrah anayecheza winga amefunga mabao 9, assist mbili katika mechi 14 alizocheza kwenye klabu ya Benchima