ISMAIL MHESA AITOSA MASHUJAA
Winga wa Kitanzania Ismail Aidan Mhesa ameachana na klabu ya Mashujaa FC ya Kigoma Baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Ismail alijiunga na Mashujaa FC mwanzoni mwa msimu huu wakati wa dirisha kubwa la Usajili na Sasa mambo hayajaenda Vizuri hivyo ameachana na klabu hiyo.
Mhesa kwasasa yuko katika mazungumzo na klabu ya Mtibwa Sugar FC ambayo alicheza kabla ya kwenda kujiunga na Mashujaa FC.