AZAM YASHINDA KWA MBINDE
Goli pekee lililofungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza na mshambuliaji bonge wa Azam FC Alassane Diao liliiwezesha matajiri hao wa Chamazi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar usiku wa leo katika michuano ya kombe la Mapinduzi.
Hiyo ni mechi ya pili kwa Azam ambao katika mchezo wao kwanza walilazimishwa sare isiyo na bao dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Mlandege