MOSES PHIRI ATIMKIA APR


Klabu ya APR ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Simba ili kuipata saini ya mshambuliaji raia wa Zambia, Moses Phiri kwa mkataba wa mkopo katika dirisha hili dogo la uhamisho la msimu huu.

Kwa mujibu wa Abdelhak Benchikha ameuambia Uongozi wa Simba kuwa anahitaji kufanya kazi na wachezaji wenye umri mdogo huku Moses Phiri hayupo kwenye mipango yake ya kuitengeneza timu bora.

Taarifa za kuaminika ni kuwa Moses Phiri amekubali kujiunga na APR baada ya klabu hiyo kuiomba Simba kumtoa kwa mkopo Moses Phiri na Simba haitarajii kumtoa mchezaji huyo kwenye timu iliyotwaa kombe la Ligi Kuu msimu uliopita.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI