OKRAH NI WA YANGA
Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC imemtambulisha mchezaji wake mpya Augustine Okrah atakayeitumikia klabu hiyo kuanzia sasa hadi 2026 mkataba wake utakapomalizika.
Okrah amejiunga na Yanga akitokea klabu ya Bemchem ya Ghana aliyojiunga nayo msimu uliopita akitokea Simba SC ambao ni mahasimu wa Yanga.
Usajili wa Okrah unaweza kuwaliza watani zao kwani mchezaji aliondoka klabuni hapo akidaiwa ni mgonjwa na pia ni mtovu wa nidhamu, jambo ambalo si kweli