YANGA YAENDELEZA 5 HADI KOMBE LA MAPINDUZI
Yanga SC imewapa zawadi ya kuaga mwaka wa 2023 kwa kuendeleza vipigo vyake vya mabao matano, hasa baada ya usiku huu kuifumua Jamhuri ya Pemba mabao 5-0 katika uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.
Ushindi huo mkubwa wa kombe la Mapinduzi umeifanya Yanga kuweka hai matumaini yake ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Crispin Ngushi aliyefunga mawili, Kibwana Shomari, Walid Mzize na Skudu Makulubela