USHAURI WA ALLY KAMWE KWA AHMED ALLY
Shida ni kwamba Timu inaposhinda Msemaji unajimilikisha ushindi huo. Unatamba nao na kujipa kila aina ya majina kuonyesha kwamba Wewe ni KILA KITU kwenye Ushindi.
Lakini timu inapopata matokeo mabaya, Unajitenga nayo. Unaanza kutupa lawama hadharani kwa wachezaji kuwa hawana Ubora na Uchu wa kuipa Timu mafanikio.. Huku ni KUKOSA HESHIMA.
Ni Ubinafsi na unaonyesha ni kwa kiasi gani Msemaji upo kwa ajili ya kulijenga jina lako na sio kuijenga Taasisi yako. Na hii ni mbaya pindi Interest binafsi zinapotangulia kuliko Interest za Taasisi.
Jambo moja ambalo inatupasa tuelewe, Nyakati nzuri na mbaya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mchezaji anayekwenda uwanjani ili apoteze mchezo.
Kuwazodoa na kuwasema hadharani wachezaji wako ni kutaka kuwachonganisha na mashabiki. Ni ishara pia ya kutoheshimu kazi yao.
Na hata inapobidi, wachezaji wakatakiwa kusemwa, mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Benchi la Ufundi, Sio msemaji wa Timu.
Makocha wamekaa Darasani na wakafundishwa jinsi ya kuishi na kuwaelekeza wachezaji. Tuache wafanye kazi yao.
Kuwa Msemaji haimaanishi Wewe Unajua kila kitu. Haimaanishi una nguvu na uwezo wa kukosoa wapambanaji wako Public. Tujue mipaka yetu.
Kesho na keshokutwa wachezaji wakianza kutukanwa mitandaoni na kupigwa mawe na mashabiki barabarani, Tutaanza kusema kuwa tuna mashabiki wapuuzi.. Kumbe ‘Upuuzi’ tunaujenga kwa vinywa vyetu wenyewe..
Huwezi kuonekana Smart kwa kukosoa na kuwasema wachezaji hadharani .. ili kufurahisha kikundi cha watu wachache..
Hii ni mbaya sana, utamalizana na wachezaji kisha kesho utawakosoa viongozi wenzako na kisha utahamia kwa mashabiki.. Mwisho wake huwa mbaya sana.
Tubadilike .. Kinachotupa Umaarufu na majina makubwa mjini ni TIMU sio Vinywa vyetu .. Tujifunze kuheshimu na kuwalinda wachezaji wetu.
Mwenyekiti wa Wasemaji Hapa ..
Ally Kamwe ✍🏻