Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2023

MBWANA SAMATTA ANUKIA MISRI

Picha
Al-Ahly ya Misri imeripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta wakati huu wa usajili Vigogo hao wa Cairo kwa sasa wanatafuta mshambuliaji wa kati na chaguo lao la kwanza ni Mkongomani Jackson Muleka. Hata hivyo, Muleka anayekipiga na Besiktas anadaiwa kutaka kiasi kikubwa cha fedha kujiunga na miamba hiyo barani Afrika. Lakini endapo watamkosa, bado jicho lao la pili lipo kwa Samatta anayekipiga na Genk, Kwa mujibu wa Sporx, Krc Genk, wana mpango wa kumuuza Samatta, kwa Dola 3Milioni zadi ya Bilioni 7 za Tanzania Genk wanataka kumuuza Samatta ila huko Ulaya sio Africa Samatta anaripotiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 2.7. Kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe aliyewahi pia kuichezea Aston Villa akajiunga na timu hiyo kwa sababu Al- Ahly wanahitaji kuwa na mshambuliaji wa kati mapema iwezekanavyo kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia la vilabu linaloanza mwezi ujao.

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA JULAI 1

Picha
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF ) limetangaza tarehe ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili la msimu 2023-24, ambapo siku ya kesho dirisha hilo litafunguliwa.

TEAM JOB YAIKANDIKA 4-2 TEAM KIBWANA

Picha
Timu iliyohusisha upande wa Dickson Job jioni ya leo imeichapa timu ya upande wa Kibwana Shomari wote ni wachezaji wa Yanga mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Hisani uliopigwa mjini Morogoro. Mabao mawili ya Abdul Sopu dakika ya 23 na 50 na mawili ya Simon Msuva dakika 74 na 80 yalihitimisha mchezo huo kabla ya changamoto za penalti zilipofanikisha mchezo huo wa Hisani

SELEMAN MATOLA KUMRITHI MINZIRO GEITA GOLD

Picha
Uongozi wa Klabu ya Geita Gold FC umetaja jina la Kocha Suleimani Matola kama mtu sahihi kukabidhiwa timu kwa kipindi hiki baada ya Minziro kumaliza mkataba wake Klabuni hapo. Geita hawana Kocha mkuu hadi sasa na Kocha anyepigiwa hesabu ni Matola ambaye majuma kadhaa nyuma ametoka kutambulishwa kuwa Kocha wa timu za Vijana za Simba U-17 na U-20.

JUMA MGUNDA KUREJEA COASTAL UNION

Picha
Taarifa kutoka Coastal Union ya Tanga ,uongozi wa Klabu hiyo unampango wa kumrudisha aliyekuwa Kocha wao Juma Mgunda ikiwa ni siku chache baada ya kuvunja benchi lote la ufundi la timu yao . Simba SC walipanga kumkabidhi Kocha Juma Mgunda timu ya Wanawake Simba Queens kuelekea msimu ujao, lakini taarifa zilizotoka hii leo ni kuwa huwenda Juma Mgunda akarudi kwa Mabosi wake wa zamani .

PETER BANDA AISHIKA PABAYA SIMBA, ATAKA MAMILIONI KUVUNJA MKATABA

Picha
Menejimenti ya Royal Soccer Scout Management inayomsimamia Winga wa Klabu ya Simba,Peter Banda imeuambia Uongozi wa Simba kuwa hautaki mteja wao apelekwe kwa mkopo Klabu yoyote ile na badala yake ni kuchagua kumvunjia Mkataba wake na kumlipa pesa zake au kumhakikishia nafasi ya kucheza mda mwingi kuelekea Msimu ujao. Banda ambaye kwa sasa yupo nchini kwao Malawi anaamini uwezo wa kucheza kwenye Kikosi cha Simba upo ndio maana anashinikiza kuvunjiwa Mkataba ili akacheze sehemu Nyingine au kuhakikishiwa nafasi ya kucheza hali ambayo imewagawa viongozi wa Simba na kushindwa kuafikia maamuzi juu yake. .

MASTAA WA ZAMANI SIMBA WAMTAMBIRIA MAKUBWA MKUDE AKIWA YANGA

Picha
"Sioni sababu ya kuipumzisha jezi eti hadi apatikane mchezaji mwingine kutoka timu ya vijana, asipopatikana mwenye ubora kama Mkude ina maana haitatumika milele, jezi zinazowekwa kando kikawaida ni zile za wachezaji waliofariki kama Patrick Mafisango ili mashabiki wasikumbuke machungu" "Nawashauri tu viongozi wa Simba watulie kwenye maamuzi yao kwa sasa, waache wachezaji kwa sababu za msingi na wasajili ambao kweli watakuwa na msaada na timu yao," GEORGE MASATU,Beki wa zamani wa Klabu ya Simba SC. "Wanaiweka kando jezi ili iweje?, Hakuna sababu ila naona ni siasa zinaendelea ndani ya Simba, namna walivyomuacha wamekosea hivyo wanatafuta namna ya kujisafisha, waache jezi itumike na mchezaji mwingine. "Binafsi naona Mkude atafanya vizuri huko atakapowenda na sidhani hayo mambo yao ya kumuaga kama yatafanikiwa endapo atasaini Yanga kweli, Yanga hawawezi kumruhusu kwenda kuagwa na hakuna sababu kwasasa, Simba hawajamheshimu Mkude," EMMANUELI GABRIEL, Msha...

BERNARD MORRISON KUIBUKIA AZAM

Picha
INASEMEKANA kiungo mshambuliaji wa zamani wa miamba Simba na Yanga Bernard Morrison anatarajia kutambulishwa na wanalamba lamba, Azam FC. Inadaiwa kwamba Bernard Morrison amejiunga na Azam fc kwa mkataba wa miaka miwili ,

YANGA YAMALIZANA NA LUC EYMAEL

Picha
"Klabu tumeshafanya mawasiliano na kocha, Luc Eymael na ameshalipwa awamu hii kwa mujibu wa makubaliano. Tumeshawasiliana na (FIFA) pia kuwajulisha hilo" "Mengine ni propaganda tu za kutengeneza taharuki kwa mashabiki wetu. Kwa 90% tayari wachezaji waliohitajika, wameshasaini mikataba na sasa bado kuwatambulisha tu" "Tukimaliza kuzindua jezi wiki ijayo, Wananchi watafurahi vyuma vitakavyoshuka. Tunajua kuna watu wanaogopa ndio maana wanaanzisha propaganda"

PROFESA NABI AANGUKIA FAR RABAT, MOROCCO

Picha
Profesa Nabi alikuwa anatakiwa na Kaizer Chief mwisho wa siku mambo yameenda kombo zakikachero kabisa zinaeleza walishindwana. Sasa kwa mujibu wa tetesi zinaeleza Mabingwa wa Morrocco klabu ya AS FAR Rabat wanahitaji huduma ya Nabi kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya kiamataifa.

NYOTA SIMBA QUEENS AISHUTUMU POLISI

Picha
Mchezaji wa timu ya Wanawake ya Simba (Simba Queens), Jentrix Shikangwa raia wa Kenya ametupa lawama kwa jeshi la polisi nchini Kenya kwa kuzuia zawadi zake alizozipata katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania. Kupitia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Shikangwa ameandika "Nina furaha na huzuni sana kwa wakati mmoja mwezi huu nilipewa heshima ya kupokea tuzo ya kiatu cha dhahabu na kujumuishwa miongoni mwa wachezaji bora katika timu ya msimu katika msimu uliomalizika wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania lakini sikuweza kutwaa (kuchukua) tuzo zangu kwani nilikuwa nafanyia kazi baadhi ya mambo binafsi" "Kwa hivyo kwa kuwa sikuweza kuchukua, tuzo zilitumwa kama kifurushi kupitia Tahmeed ambayo iliweza kufika (27/06/2023) karibu 12PM. Kwa hivyo nilimwomba Shemeji yangu (Mume wa dada yangu) kwenda kuzichukua kwa niaba yangu ofisi za Tahmeed jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani, walimbeba wakampeleka kituo cha Polisi cha Kamukinji wakimuuliza alitoa wapi hivyo vitu...

HUYU NDIO FISTON KALALA MAYELE

Picha
HUYU ni mshambuliaji wa Yanga ambaye amekuwa akifanya vizuri msimu huu akitokea DR Congo, ndiye mfungaji bora kwenye Ligi Kuu bara.  Mayele alifikisha mabao 17 sawa na Said Ntibanzokiza wa Simba, lakini pia aliibuka kinara wa mabao katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika akifunga magoli 7 na akitoa assist 3.  Mayele anaishi kwenye apartment maeneo ya Victoria Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Sehemu ambayo mchezaji huyo anakaa na familia yake na analipa dola 800 ambayo ni sawa na shilingi milioni 1.8, ana gari kali aina ya Toyota Harrier nyeusi premio

MSUVA AZIITA SIMBA NA YANGA MEZANI

Picha
Nimemaliza mkataba kwenye timu yangu ya Saudi Arabia [nilisaini mwaka mmoja] kwa hiyo sasa hivi naangalia sehemu nyingine lakini kama na wao watanihitaji basi tutarudi mezani kuzungumza, kwa sasa mimi ni mchezaji huru! Natamanisha. Tayari ofa zimekuja lakini bado hakuna timu ambayo tumefikia makubaliano ila ofa nyingi zinatoka kwenye timu za bara la Asia japo hata Afrika pia zipo lakini kwa hapa nyumbani bado sijapokea ofa kutoka timu yoyote. Kwa sasa nisiwe muongo, bado nataka kucheza nje na kuna asilimia nyingi nitaendelea kucheza nje. Nyumbani nitarejea lakini sio kwa sasa.

DIAMOND PLATINUMZ KUACHIA NGOMA MPYA JULAI

Picha
"Julai ni mwezi wa kuzaliwa kwa mama yangu, na kuanzia mwezi huo itaanza rasmi mvua ya mawe, zangu collabo za nje na za ndani na nitahudumu hapo kwa No 1 on trend kuanzia Julai 2023 hadi January 2024, nitampisha msanii wangu mpya Wasafi na ninaoheshimiana nao" "Wakati naanza movements za kutoka nje ya East Africa wengi mlichelewa kunielewa na mkaanza kusema ooh nimeishiwa utunzi, ooh naimba ujinga, na kashfa kibao mkaanza kuwapa vichwa wasanii wasio levo yangu washindane nami, kuja kushtuka nawaletea matuzo ya kimataifa na kujaza viwanja kwenye mataifa ambayo mlizoea kuyasoma kwenye geography....huku wasanii wenu wakiwa wanasubiri matamasha ya Radio!" "Hivyo, kama mlivyokaa kwa kutulia wakati natega mabomu yangu ya kutoka nje ya East Africa, naomba pia mkae kwa kutulia vivo hivyo ninapoanza mashambulizi yangu, sitaki maoni wala ushauli ushuzi!, ushauli pelekeni Angaza, kama washauli wazuri wakati nilivyokuwa kimya nikidili na media mngewashauli hao wasanii wenu...

GEORGE MPOLE APELEKWA KITAYOSCE KWA MKOPO

Picha
George Mpole, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Kitayosce ya Tabora kwa mkopo akitokea FC Lupopo Mpole hajawa na wakati mzuri tangu asajiliwe na klabu hiyo ya DR Congo George Mpole ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara 2021/2022, yuko nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko.

ISSOUFOU SELLSAVON DAYO KUZIBA PENGO LA ONYANGO SIMBA

Picha
Klabu ya Simba inawinda saini ya beki wa kati wa Burkina Faso Issoufou Sellsavon Dayo. Dayo mwenye umri wa miaka 31 anaitumikia Klabu ya RS Berkane, ujio wa Dayo unakwenda kuziba pengo la Joash Onyango aliyeomba kuachwa

SIMBA YAMNASA KOCHA WA MAKIPA WA YANGA

Picha
Na Shafih Matuwa WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wameendelea kuimarisha benchi lake la ufundi kwa ajili ya msimu ujao hasa baada ya kumuajiri aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu ya Yanga Razack Siwa raia wa Kenya.  Wekundu hao wa Msimbazi imempa mkataba wa miaka miwili kocha huyo aliyefanya vizuri akiwa na kikosi cha Yanga wakati ule ikiwa chini ya bilionea Yusuph Manji.  Siwa atawasimamia vema makipa wa Simba na kusimama imara langoni kama ilivyokuwa kwa makipa Ally Mustapha "Barthez" na Deogratus Munishi "Dida" ambao wote kwa pamoja walinolewa na kocha huyo

MORICE CHUKWU AAGA RASMI RIVERS UNITED

Picha
Kiungo wa Rivers United United ya Nigeria Morice Chukwu anondoka rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka miwili na nusu ndani ya klabu hiyo akitokea Akwa United. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka nchini Nigeria  vinaripoti kwamba kiungo huyo ana ofa mbili kutoka Afrika Mashariki na kuna asilimia kubwa akacheza NBC Premier Legue Msimu ujao 

HARMONIZE KAFILISIKA- H- BABA

Picha
Msanii wa Muziki wa Bongofleva, H Baba amesema tangu aondoke kwenye lebo ya Konde Gang kiwango cha kimuziki cha lebo hiyo kimezidi kudidimia siku hadi siku kwasababu yeye ndiye alikuwa kinara wa kuiendesha na kuipa nguvu lebo hiyo, amesema kipindi yupo Konde Gang alikuwa anatumia nguvu nyingi kuichangamsha lebo hiyo ili ionekane ipo juu lakini ukweli ni kwamba lebo ya Konde Gang ni moja ya lebo masiki na siku za hivi karibuni itakufa kabisa. Yote tisa, kumi zilipendwa huyo wa Konde Gang amesema siyo wasanii wa Konde Gang tu ambao wameanguka kimziki, hadi Harmonize amefifia kiasi cha kufanya Show za Birthday, Harusi na Kitchen Party anazofanya huko London ambako ndiko alipo sasa hivi, ambapo amesema kwasasa Harmonize amefulia kiasi cha kushindwa kum-meneji hata Ibrah msanii pekee aliyebaki kwenye lebo hiyo. H Baba amesema Angella amepitia mambo mazito sana ambayo kwenye mahojiano yake na Millard Ayo hakuyaongea hata robo, ameamua kufunika kombe ili maisha mengine yaendelee, lakini kama...

YANGA YAMALIZANA NA KIBABAGE

Picha
Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto wa Singida Fountain Gate FC, Nickson Kibabage kwa mkataba wa miaka mitatu. Kibabage (22) Alikuwa pendekezo la kocha Nabi ambapo amepitishwa na kocha mpya wa klabu hiyo Miguel Ángel Gamondi. Nickson Kibabage Aliwahi kupita Katika Vilabu vya Mtibwa Sugar, KMC FC.

KOCHA WA MASHUJAA AFUNGIWA MSIMU MZIMA

Picha
Kocha wa Magolikipa wa timu ya Mashujaa FC Shomari Ndizi amefungiwa kwa msimu mzima wa 2023/24 kushiriki michezo yote ya ligi na mashindano yote yaliyo chini ya TFF na pia ametozwa faini ya Tsh Milioni mbili kwa kosa la kumpiga ngumi usoni kocha Mkuu wa klabu ya Mbeya City Abdallah Mbiru wakati wachezaji wa akiba na benchi la ufundi la Mashujaa wakishangilia bao walilofunga kwenye mchezo wa mtoano wa mkondo wa pili wa kuwania kucheza ligi kuu uliochezwa jijini Mbeya. Adhabu hii ni kwa kuzingatia kanuni ya 45:2(2:1) ya championship kuhusu udhibiti wa makocha.

KAIZER CHIEF YAMTOSA NABI, YATAMBULISHWA MWINGINE

Picha
Klabu ya soka ya Kaizer Chiefs imemtangaza Molefi Ntseki kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo kuanzia sasa. Awali klabu hiyo ilihusishwa na kumhitaji kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi na kuondoka kwake Yanga kulihusishwa na vigogo hao wa Afrika Kusini.

MKATABA WA MKIDE YANGA WAVUJA

Picha
Na Salum Fikiri Jr IMEFAHAMIKA kwamba mkataba wake na klabu ya Yanga aliosaini nao juzi wa mwaka mmoja umevuja, Jonas Gerrald Mkude amesaini mkataba akiwa kama mchezaji huru umevuja na inasemekana watu wake wa karibu wamevujisha mkataba huo. Kiungo huyo aliyehudumu Simba kwa mafanikio anatajwa kujiunga Yanga msimu ujao, chanzo chetu kimetuambia kuwa baada ya Simba kumtupia virago vyake na kumpa Thank you kwenye vyombo vya habari. Mchezaji huyo alianza kwa kufuatwa na watu wake wa karibu na kumpeleka Yanga. Inadaiwa kwamba Yanga iliamua kumchukua Mkude kwa sababu inaamini kuwa Mkude bado ana kiwango kikubwa isipokuwa alichokwa na watu wa Simba na wakaanza kumtengenezea chuki ili wamuondoe kikosini. Inadaiwa kwamba Mkude alisukiwa njama za kumtoa muda mrefu lakini aliweza kushinda majaribu. Yanga imempa mkataba mfupi wa mwaka mmoja lakini itamuongezea endapo itaridhishwa na kiwango chake, Yanga iliamua kusitisha mpango wa kumsajili kiungo mkabaji wa Singida Fountain Gate Yusuph Kagoma il...

DANIEL AMOAH AONGEZA MMOJA AZAM

Picha
Klabu ya Azam FC imetangaza kumwongezea Mkataba wa Mwaka mmoja beki wake wa Kimataifa wa Ghana, Daniel Amoah ambapo utamfanya kusalia Klabuni hapo mpaka June 30,2025 Beki huyo mwenye umri wa Miaka 25 Msimu huu amefanikiwa kucheza Mechi 25 za Ligi Kuu akiwa na Azam FC na kufunga magoli mawili na kadi nne za njano..

KIPA LA MPIRA TANZANIA PRISONS AAGA UKAPERA

Picha
Mchezaji Benedict Tinoco (golikipa) wa Tanzania Prisons amemvisha pete ya uchumba Martha Mboya katika Kijiji cha Marangu mkoani Kilimanjaro. Tinoco na mchumba wake wana mtoto wa kike anayeitwa Regina Tinoco mwenye umri wa miaka mitatu (3) na miezi miwili (2).

KONDE GANG HAKUNA MSANII MWENYE GARI LAKE BINAFSI- CHEED

Picha
Aliyekuwa msanii wa Konde Music Worldwide, Cheed amedai kuwa hakuna msanii wa Lebo hiyo ambaye amewahi kuwa na gari lake kama inavyoonekana mtandaoni. Utakunbuka Cheed aliachana na lebo hiyo mwaka jana pamoja na wasanii wenzake, Country Boy, Killy na Anjella. "Hakuna msanii wa Konde Gang ambaye anamiliki gari, hicho ndicho kitu ambacho unatakiwa ukijue. Sio msanii, sio mfanyikazi, ukikuta gari pale ni la ofisi". "Wewe utalitumia kwenda studio, kwenda mahojiano lakini hiyo ni mali ya kampuni,” amesema Cheed akiongea na East Africa Radio. Kwa sasa Konde Music imesalia na msanii mmoja tu ambaye ni Ibraah, huyu pia ndiye alikuwa wa kwanza kusainiwa.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AIFAGILIA SIMBA

Picha
“Kwa hiki ninachokiona sasa, naamini Simba itakuwa imara zaidi msimu ujao. Niliangalia mchezo dhidi ya Wydad Casablanca tuliwatoa jasho kule kwao, kuna vitu vidogo tunatakiwa kuviongeza. Kama kuna vitu vinahitajika kwa ajili ya jambo hilo tuko tayari kusaidia,” Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani.

SIMBA KUISTAAFISHA JEZI NAMBA 20 YA MKUDE

Picha
Klabu yetu ya Simba SC imestaafisha jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa kiungo wetu Jonas Gerald Mkude ‘Nungunungu’ uamuzi ambao ni sehemu ya heshima ambayo viongozi wetu wameamua kumpa nyota huyo baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 13. Mkude ambaye alitokea kwenye shule ya vijana ya Simba SC na kudumu katika kikosi cha wakubwa kwa takribani miaka 13 ameondoka klabuni Simba Sc baada ya mkataba wake kufikia ukomo. Jezi namba 20 haitakuwepo msimu ujao hadi pale atakapopatikana mhitimu mwingine mwenye kuakisi kile ambacho Mkude amefanya klabuni hapo. Aidha klabu yetu imepanga kumfanyia makubwa @jonasmkude20 ikiwa ni kumuaga kwa heshima siku ya Simba Day 2023, Inayotarajiwa kufanyika August 8,8,2023, huku ikimpa nafasi ya kurejea klabuni hapo baada ya maisha ya kucheza mpira kama ilivyo kwa Mussa Hassan Mgosi.

DICKSON JOB NA MWAMNYETO WAJA NA FOUNDATION YAO

Picha
Taasisi ya Mwamnyeto Foundation ambayo imeanzishwa na wachezaji wawili wa Young Africans Sports Club, Bakari Nondo Mwamnyeto na Gift Mauya imeandaa matamasha mawili yatakayofanyika katika mikoa miwili tofauti [Tanga na Morogoro] lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii yenye uhitaji maalum. Tamasha la kwanza litafanyika Julai 2, 2023 Mkoani Tanga ambako Mwamnyeto anatokea, halafu Julai 7, 202 litafanyika Morogoro ambako ni nyumbani kwa Mauya. Matamasha yote mawili yatahusisha mambo mawili, jambo la kwanza ni kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji maalum halafu jambo la pili itakuwa ni mechi ambayo itahusisha timu itakayoundwa na Mwamnyeto na Mauya na watu wao dhidi ya combine ya Mkoa wa Tanga pamoja na Morogoro.

KVC WESTERIO YA UBELGIJI YAIPA SIMBA BIL 1.5 KUMNUNUA SAKHO

Picha
Na Ikram Khamees. KLABU ya KVC Westerio ya Ubelgiji inayoshiriki Ligi Kuu imeweka mezani shilingi bilioni 1.5 za Kitanzania ili kumnyakua kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal. Kwa mujibu wa Mambo Uwanjani Blog, kvc imetuma wawakilishi wake mitaa ya Msimbazi ili kumnasa nyota huyo, klabu hiyo ilianza kumfuatilia Sakho tangu msimu uliopita ambapo alishinda tuzo ya goli bora la Shirikisho la soka, CAF. Licha kwamba msimu huu hakuwa na nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, lakini KVC wanaitaka huduma yake

ROYAL TOUR YA MAMA SAMIA INALIPA AISEE, BEKI LA PSG NA MKEWE NDANI YA SERENGETI

Picha
Beki wa PSG Mfaransa Layvin Kurzawa pamoja na mpenzi wake Melissa Chovet wametembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania wakati huu ambao wapo likizo.

AISHI MANULA YUPO KIJIJINI MKAMBA

Picha
Kipa wa Simba SC Aishi Manula akiwa Nyumbani kwao Mkamba Kirombero mkoani Morogoro katika kipindi hichi cha mapumziko lakini pia akiendelea kujiuguza jeraha lake baada ya kufanyiwa operation. "Ni ardhi yenye kuponya na kutia nguvu, Niwapo hapa najiona mwenye Furaha na amani. Sijawahi kuwa mnyonge ninapokuwa nyumbani kwa baba alipotuacha na mama" Kipa wa Simba SC Aishi Manula.

HUYU NDIO FRED VUNJABEI

Picha
"Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na duka moja dogo sana Kariakoo (Goli), baada ya kujikusanya tulikubaliana na rafiki yangu Frank Knows twende kujaribu kununua mzigo China, tulisubiri kipindi cha tiketi za offer na tukapata Ethiopian Airways, tulifanikiwa kufanya utafiti wa maana sana China na tukajilaumu tulikuwa wapi siku zote, Ndoto zangu nlianza kuziona zikikamilika licha ya kuwa China ilitakiwa uwe na hela nyingi na wote tulisafiri na pesa kidogo sana hazikutosha kununua mzigo. Nilitafakari nifanye nini? hesabu zetu zilionesha kununua mzigo mdogo China ni kazi bure na hela itapotea, mwisho wa siku niliamka asubuhi nkamuita Frank nikamwambia “Nimeamua kukupa hela yangu yote ukifanikiwa utanishika mkono ukifeli tutakuwa tumejifunza kitu” alinishangaa sana, Alipojumlisha na yake jumla ikawa million kumi na mbili (12mil), Nlifanya hivyo kwa sababu zifuatazo; Moja, Nilijua lazima mmoja wetu akubali kuwa na subira na mwingine atangulie (urafiki wetu hatukuwahi kuweka wivu na ubinaf...

SIMBA MSIFUATE MKUMBO KWA KUFANYA USAJILI KISHABIKI

Picha
KUNA majina makubwa nayasikia yakitajwa kuhusishwa katika usajili wa klabu ya Simba SC, majina hayo miongoni mwao ni shinikizo la mashabiki wa Simba wakitaka wawe katika kikosi chao msimu ujao.  Mashabiki wana nguvu kubwa pengine kuliko hata wanachama na viongozi wa klabu, mashabiki pia wana nguvu kubwa pengine kuliko waandishi wa habari hasa za michezo.  Katika kipindi kama hiki cha usajili, yatazungumzwa mengi ili kila mmoja apendekeze mchezaji wake.  Kuna vijiwe vyenye ushawishi mkubwa kwenye masuala ya usajili na hata wakijadili kitu mwishowe hutokea. kuwa kweli, vijiwe vyenye nguvu kama cha Karume, Magomeni, Buguruni, Temeke, Mbezi na kwingineko, mashabiki wamekuwa na sauti kubwa wakitaka lao lazima lifanikiwe.  Klabu ya Simba inaweza kuingia kwenye mtego mkubwa kwenye dirisha hili la usajili, matajiri wa klabu hiyo wanasaka saini za wachezaji wanaopendekezwa kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.  Miongoni mwa wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu ni wale wanaopendekezwa na mashabiki wa ...

YANGA YAFUNGIWA NA FIFA

Picha
Klabu ya Yanga SC imekumbwa na adhabu ya kufungiwa kufanya usajili wa Wachezaji baada ya kushindwa kumlipa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Luc Eymael malipo yake ya kufutwa kazi. Wakili wa kocha huyo wa Ubelgiji alithibitisha taarifa hiyo baada ya uamuzi huo kuwasilishwa na FIFA siku ya Jumapili.

MKUDE AHUSISHWA NA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr BAADA ya kumkosa kiungo mkabaji Yusuph Kagoma aliyeongeza mkataba kwenye timu yake ya Singida Fountain Gate kwa miaka mitatu, mabingwa wa soka nchini Yanga SC imeamua kumnasa kiungo mkabaji Jonas Mkude aliyeachwa na Simba.  Mambo Uwanjani Blog ina uhakika kwamba Mkude atacheza msimu ujao kwenye vilabu vinne vilivyoshika nafasi ya juu {Top four}, mchezaji huyo alitajwa kutua Azam FC kabla hata msimu haujafika tamati.  Lakini leo vijiwe mbalimbali jijini Dar es Salaam zimezagaa taarifa kwamba kiungo huyo mahiri aliyeibuliwa na Simba B anatarajia kujiunga na Yanga

OKWA AFUNGUKA MAKUBWA SIMBA

Picha
Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amefunguka juu yaliyokuwa yakijiri klabuni hapo ambapo amefichua kuwa wachezaji hawachezeshwi kulingana na utendaji wao mazoezini bali ‘yupo mtu ambaye huja na orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na wasiotakiwa kucheza bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi.’ Akizungumza na kituo cha habari cha G&T Online TV, Okwa amesema, "Wakati Kocha Zoran akiwa Simba ilikuwa mchezaji unacheza kulingana na ulivyo-perfom kwenye mazoezi, lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta Orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi"

TRY AGAIN AKABIDHI JEZI KWA WABUNGE NA WADAU

Picha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amekabidhi zawadi za jezi kwa Wabunge na wadau mbalimbali wa timu yetu katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ukumbi wa LAPF Dodoma ikiwa ni kuthamini mchango wao kwa klabu.