KOCHA WA MASHUJAA AFUNGIWA MSIMU MZIMA
Kocha wa Magolikipa wa timu ya Mashujaa FC Shomari Ndizi amefungiwa kwa msimu mzima wa 2023/24 kushiriki michezo yote ya ligi na mashindano yote yaliyo chini ya TFF na pia ametozwa faini ya Tsh Milioni mbili kwa kosa la kumpiga ngumi usoni kocha Mkuu wa klabu ya Mbeya City Abdallah Mbiru wakati wachezaji wa akiba na benchi la ufundi la Mashujaa wakishangilia bao walilofunga kwenye mchezo wa mtoano wa mkondo wa pili wa kuwania kucheza ligi kuu uliochezwa jijini Mbeya.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia kanuni ya 45:2(2:1) ya championship kuhusu udhibiti wa makocha.