MSUVA AZIITA SIMBA NA YANGA MEZANI
Nimemaliza mkataba kwenye timu yangu ya Saudi Arabia [nilisaini mwaka mmoja] kwa hiyo sasa hivi naangalia sehemu nyingine lakini kama na wao watanihitaji basi tutarudi mezani kuzungumza, kwa sasa mimi ni mchezaji huru! Natamanisha.
Tayari ofa zimekuja lakini bado hakuna timu ambayo tumefikia makubaliano ila ofa nyingi zinatoka kwenye timu za bara la Asia japo hata Afrika pia zipo lakini kwa hapa nyumbani bado sijapokea ofa kutoka timu yoyote.
Kwa sasa nisiwe muongo, bado nataka kucheza nje na kuna asilimia nyingi nitaendelea kucheza nje. Nyumbani nitarejea lakini sio kwa sasa.