OKWA AFUNGUKA MAKUBWA SIMBA
Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amefunguka juu yaliyokuwa yakijiri klabuni hapo ambapo amefichua kuwa wachezaji hawachezeshwi kulingana na utendaji wao mazoezini bali ‘yupo mtu ambaye huja na orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na wasiotakiwa kucheza bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi.’
Akizungumza na kituo cha habari cha G&T Online TV, Okwa amesema, "Wakati Kocha Zoran akiwa Simba ilikuwa mchezaji unacheza kulingana na ulivyo-perfom kwenye mazoezi, lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta Orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi"