SELEMAN MATOLA KUMRITHI MINZIRO GEITA GOLD
Uongozi wa Klabu ya Geita Gold FC umetaja jina la Kocha Suleimani Matola kama mtu sahihi kukabidhiwa timu kwa kipindi hiki baada ya Minziro kumaliza mkataba wake Klabuni hapo.
Geita hawana Kocha mkuu hadi sasa na Kocha anyepigiwa hesabu ni Matola ambaye majuma kadhaa nyuma ametoka kutambulishwa kuwa Kocha wa timu za Vijana za Simba U-17 na U-20.