MKATABA WA MKIDE YANGA WAVUJA
Na Salum Fikiri Jr
IMEFAHAMIKA kwamba mkataba wake na klabu ya Yanga aliosaini nao juzi wa mwaka mmoja umevuja, Jonas Gerrald Mkude amesaini mkataba akiwa kama mchezaji huru umevuja na inasemekana watu wake wa karibu wamevujisha mkataba huo.
Kiungo huyo aliyehudumu Simba kwa mafanikio anatajwa kujiunga Yanga msimu ujao, chanzo chetu kimetuambia kuwa baada ya Simba kumtupia virago vyake na kumpa Thank you kwenye vyombo vya habari.
Mchezaji huyo alianza kwa kufuatwa na watu wake wa karibu na kumpeleka Yanga. Inadaiwa kwamba Yanga iliamua kumchukua Mkude kwa sababu inaamini kuwa Mkude bado ana kiwango kikubwa isipokuwa alichokwa na watu wa Simba na wakaanza kumtengenezea chuki ili wamuondoe kikosini.
Inadaiwa kwamba Mkude alisukiwa njama za kumtoa muda mrefu lakini aliweza kushinda majaribu.
Yanga imempa mkataba mfupi wa mwaka mmoja lakini itamuongezea endapo itaridhishwa na kiwango chake, Yanga iliamua kusitisha mpango wa kumsajili kiungo mkabaji wa Singida Fountain Gate Yusuph Kagoma ili waweze kumsajili kiungo huyo anayekumbukwa na wanasimba.
Kwa kifupi Yanga kama imeokota pochi chini ya muembe kwani Mkude si wa kumchukua bure ilipaswa Yanga kumnunua kwa mamilioni