KVC WESTERIO YA UBELGIJI YAIPA SIMBA BIL 1.5 KUMNUNUA SAKHO
Na Ikram Khamees. KLABU ya KVC Westerio ya Ubelgiji inayoshiriki Ligi Kuu imeweka mezani shilingi bilioni 1.5 za Kitanzania ili kumnyakua kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal.
Kwa mujibu wa Mambo Uwanjani Blog, kvc imetuma wawakilishi wake mitaa ya Msimbazi ili kumnasa nyota huyo, klabu hiyo ilianza kumfuatilia Sakho tangu msimu uliopita ambapo alishinda tuzo ya goli bora la Shirikisho la soka, CAF.
Licha kwamba msimu huu hakuwa na nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, lakini KVC wanaitaka huduma yake