MKUDE AHUSISHWA NA YANGA
Na Salum Fikiri Jr
BAADA ya kumkosa kiungo mkabaji Yusuph Kagoma aliyeongeza mkataba kwenye timu yake ya Singida Fountain Gate kwa miaka mitatu, mabingwa wa soka nchini Yanga SC imeamua kumnasa kiungo mkabaji Jonas Mkude aliyeachwa na Simba.
Mambo Uwanjani Blog ina uhakika kwamba Mkude atacheza msimu ujao kwenye vilabu vinne vilivyoshika nafasi ya juu {Top four}, mchezaji huyo alitajwa kutua Azam FC kabla hata msimu haujafika tamati.
Lakini leo vijiwe mbalimbali jijini Dar es Salaam zimezagaa taarifa kwamba kiungo huyo mahiri aliyeibuliwa na Simba B anatarajia kujiunga na Yanga