MASTAA WA ZAMANI SIMBA WAMTAMBIRIA MAKUBWA MKUDE AKIWA YANGA
"Sioni sababu ya kuipumzisha jezi eti hadi apatikane mchezaji mwingine kutoka timu ya vijana, asipopatikana mwenye ubora kama Mkude ina maana haitatumika milele, jezi zinazowekwa kando kikawaida ni zile za wachezaji waliofariki kama Patrick Mafisango ili mashabiki wasikumbuke machungu"
"Nawashauri tu viongozi wa Simba watulie kwenye maamuzi yao kwa sasa, waache wachezaji kwa sababu za msingi na wasajili ambao kweli watakuwa na msaada na timu yao,"
GEORGE MASATU,Beki wa zamani wa Klabu ya Simba SC.
"Wanaiweka kando jezi ili iweje?, Hakuna sababu ila naona ni siasa zinaendelea ndani ya Simba, namna walivyomuacha wamekosea hivyo wanatafuta namna ya kujisafisha, waache jezi itumike na mchezaji mwingine.
"Binafsi naona Mkude atafanya vizuri huko atakapowenda na sidhani hayo mambo yao ya kumuaga kama yatafanikiwa endapo atasaini Yanga kweli, Yanga hawawezi kumruhusu kwenda kuagwa na hakuna sababu kwasasa, Simba hawajamheshimu Mkude,"
EMMANUELI GABRIEL, Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Simba SC.
.