SIMBA YAMNASA KOCHA WA MAKIPA WA YANGA

Na Shafih Matuwa

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wameendelea kuimarisha benchi lake la ufundi kwa ajili ya msimu ujao hasa baada ya kumuajiri aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu ya Yanga Razack Siwa raia wa Kenya. 

Wekundu hao wa Msimbazi imempa mkataba wa miaka miwili kocha huyo aliyefanya vizuri akiwa na kikosi cha Yanga wakati ule ikiwa chini ya bilionea Yusuph Manji. 

Siwa atawasimamia vema makipa wa Simba na kusimama imara langoni kama ilivyokuwa kwa makipa Ally Mustapha "Barthez" na Deogratus Munishi "Dida" ambao wote kwa pamoja walinolewa na kocha huyo


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA