TEAM JOB YAIKANDIKA 4-2 TEAM KIBWANA
Timu iliyohusisha upande wa Dickson Job jioni ya leo imeichapa timu ya upande wa Kibwana Shomari wote ni wachezaji wa Yanga mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Hisani uliopigwa mjini Morogoro.
Mabao mawili ya Abdul Sopu dakika ya 23 na 50 na mawili ya Simon Msuva dakika 74 na 80 yalihitimisha mchezo huo kabla ya changamoto za penalti zilipofanikisha mchezo huo wa Hisani