DIAMOND PLATINUMZ KUACHIA NGOMA MPYA JULAI


"Julai ni mwezi wa kuzaliwa kwa mama yangu, na kuanzia mwezi huo itaanza rasmi mvua ya mawe, zangu collabo za nje na za ndani na nitahudumu hapo kwa No 1 on trend kuanzia Julai 2023 hadi January 2024, nitampisha msanii wangu mpya Wasafi na ninaoheshimiana nao"

"Wakati naanza movements za kutoka nje ya East Africa wengi mlichelewa kunielewa na mkaanza kusema ooh nimeishiwa utunzi, ooh naimba ujinga, na kashfa kibao mkaanza kuwapa vichwa wasanii wasio levo yangu washindane nami, kuja kushtuka nawaletea matuzo ya kimataifa na kujaza viwanja kwenye mataifa ambayo mlizoea kuyasoma kwenye geography....huku wasanii wenu wakiwa wanasubiri matamasha ya Radio!"

"Hivyo, kama mlivyokaa kwa kutulia wakati natega mabomu yangu ya kutoka nje ya East Africa, naomba pia mkae kwa kutulia vivo hivyo ninapoanza mashambulizi yangu, sitaki maoni wala ushauli ushuzi!, ushauli pelekeni Angaza, kama washauli wazuri wakati nilivyokuwa kimya nikidili na media mngewashauli hao wasanii wenu mnaowashindanisha wayafanye hata robo ya nilichokuwa nafanya kwenye matuzo, majukwaa kupunguza hizi zarau za Wanigeria leo, lakini wote viliwashinda, asa wanaume tunao yaweza tunapoyaanza tunaomba mtulize K!"- ameandika Diamond Platnumz.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA