SIMBA MSIFUATE MKUMBO KWA KUFANYA USAJILI KISHABIKI
KUNA majina makubwa nayasikia yakitajwa kuhusishwa katika usajili wa klabu ya Simba SC, majina hayo miongoni mwao ni shinikizo la mashabiki wa Simba wakitaka wawe katika kikosi chao msimu ujao.
Mashabiki wana nguvu kubwa pengine kuliko hata wanachama na viongozi wa klabu, mashabiki pia wana nguvu kubwa pengine kuliko waandishi wa habari hasa za michezo.
Katika kipindi kama hiki cha usajili, yatazungumzwa mengi ili kila mmoja apendekeze mchezaji wake.
Kuna vijiwe vyenye ushawishi mkubwa kwenye masuala ya usajili na hata wakijadili kitu mwishowe hutokea.
kuwa kweli, vijiwe vyenye nguvu kama cha Karume, Magomeni, Buguruni, Temeke, Mbezi na kwingineko, mashabiki wamekuwa na sauti kubwa wakitaka lao lazima lifanikiwe.
Klabu ya Simba inaweza kuingia kwenye mtego mkubwa kwenye dirisha hili la usajili, matajiri wa klabu hiyo wanasaka saini za wachezaji wanaopendekezwa kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.
Miongoni mwa wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu ni wale wanaopendekezwa na mashabiki wa Simba, majina makubwa yanaoimbwa kila kuchwao ni Luis Miquissone raia Msumbiji, Cesar Manzoki wa DR Congo na Victorien Adebayor wa Niger.
Mbali ya majina hayo, mashabiki wa
lolote mwishoni mwa msimu jambo ambalo linawasikitisha mashabiki wake, licha ya kukosa mataji ambayo watani wake Yanga SC wakifanya vizuri ikiwemo kushinda mataji yote matatu mara mbili mfululizo.
Na pia kuingia fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, mashabiki wa Simba wamechoshwa na timu yao ya Simba kutolewa kwenye robo fainali, Wekundu hao wa Msimbazi walifanikiwa kuingia robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Lakini imekuwa ikiishia hatua hiyo, Wanasimba wanasikitishwa sana na kitendo cha Simba kuishia robo fainali wakati mahasimu wao kwa mara ya kwanza kuingia robo fainali ya michuano ya CAF wakavuka hadi fainali. Hivyo kwa upande wa Simba msimu ujao na wao wana shauku kubwa angalau wafike nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika au fainali na vile vile kurejesha mataji yao ya ligi za ndani.
Ili kufanya yote yote lazima timu ifanye usajili kabambe ya wachezaji wazuri wa hapa nyumbani kwa maana wazawa na wa kigeni. Ili kupata wachezaji wazuri uongozi wa Simba wasije kuingizwa chaka na kurudia yale yale ya msimu uliopita.
ALAMSIKI.
Kwa maoni na ushauri 0755-522216