HUYU NDIO FISTON KALALA MAYELE
HUYU ni mshambuliaji wa Yanga ambaye amekuwa akifanya vizuri msimu huu akitokea DR Congo, ndiye mfungaji bora kwenye Ligi Kuu bara.
Mayele alifikisha mabao 17 sawa na Said Ntibanzokiza wa Simba, lakini pia aliibuka kinara wa mabao katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika akifunga magoli 7 na akitoa assist 3.
Mayele anaishi kwenye apartment maeneo ya Victoria Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Sehemu ambayo mchezaji huyo anakaa na familia yake na analipa dola 800 ambayo ni sawa na shilingi milioni 1.8, ana gari kali aina ya Toyota Harrier nyeusi premio