DICKSON JOB NA MWAMNYETO WAJA NA FOUNDATION YAO
Taasisi ya Mwamnyeto Foundation ambayo imeanzishwa na wachezaji wawili wa Young Africans Sports Club, Bakari Nondo Mwamnyeto na Gift Mauya imeandaa matamasha mawili yatakayofanyika katika mikoa miwili tofauti [Tanga na Morogoro] lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii yenye uhitaji maalum.
Tamasha la kwanza litafanyika Julai 2, 2023 Mkoani Tanga ambako Mwamnyeto anatokea, halafu Julai 7, 202 litafanyika Morogoro ambako ni nyumbani kwa Mauya.
Matamasha yote mawili yatahusisha mambo mawili, jambo la kwanza ni kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji maalum halafu jambo la pili itakuwa ni mechi ambayo itahusisha timu itakayoundwa na Mwamnyeto na Mauya na watu wao dhidi ya combine ya Mkoa wa Tanga pamoja na Morogoro.