MBWANA SAMATTA ANUKIA MISRI


Al-Ahly ya Misri imeripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta wakati huu wa usajili

Vigogo hao wa Cairo kwa sasa wanatafuta mshambuliaji wa kati na chaguo lao la kwanza ni Mkongomani Jackson Muleka.

Hata hivyo, Muleka anayekipiga na Besiktas anadaiwa kutaka kiasi kikubwa cha fedha kujiunga na miamba hiyo barani Afrika.

Lakini endapo watamkosa, bado jicho lao la pili lipo kwa Samatta anayekipiga na Genk,

Kwa mujibu wa Sporx, Krc Genk, wana mpango wa kumuuza Samatta, kwa Dola 3Milioni zadi ya Bilioni 7 za Tanzania Genk wanataka kumuuza Samatta ila huko Ulaya sio Africa

Samatta anaripotiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 2.7.

Kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe aliyewahi pia kuichezea Aston Villa akajiunga na timu hiyo kwa sababu Al- Ahly wanahitaji kuwa na mshambuliaji wa kati mapema iwezekanavyo kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia la vilabu linaloanza mwezi ujao.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA