HARMONIZE KAFILISIKA- H- BABA


Msanii wa Muziki wa Bongofleva, H Baba amesema tangu aondoke kwenye lebo ya Konde Gang kiwango cha kimuziki cha lebo hiyo kimezidi kudidimia siku hadi siku kwasababu yeye ndiye alikuwa kinara wa kuiendesha na kuipa nguvu lebo hiyo, amesema kipindi yupo Konde Gang alikuwa anatumia nguvu nyingi kuichangamsha lebo hiyo ili ionekane ipo juu lakini ukweli ni kwamba lebo ya Konde Gang ni moja ya lebo masiki na siku za hivi karibuni itakufa kabisa.

Yote tisa, kumi zilipendwa huyo wa Konde Gang amesema siyo wasanii wa Konde Gang tu ambao wameanguka kimziki, hadi Harmonize amefifia kiasi cha kufanya Show za Birthday, Harusi na Kitchen Party anazofanya huko London ambako ndiko alipo sasa hivi, ambapo amesema kwasasa Harmonize amefulia kiasi cha kushindwa kum-meneji hata Ibrah msanii pekee aliyebaki kwenye lebo hiyo.

H Baba amesema Angella amepitia mambo mazito sana ambayo kwenye mahojiano yake na Millard Ayo hakuyaongea hata robo, ameamua kufunika kombe ili maisha mengine yaendelee, lakini kama angemwaga mpunga hadharani hadi sasa Harmonize angekuwa dhofulihali kwa unyanyasaji aliomfanyia Angella. Staa huyo amemalizia kwa kusema yeye bado yuko WCB na hana mpango wa kuhama



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA