YANGA YAMALIZANA NA LUC EYMAEL
"Klabu tumeshafanya mawasiliano na kocha, Luc Eymael na ameshalipwa awamu hii kwa mujibu wa makubaliano. Tumeshawasiliana na (FIFA) pia kuwajulisha hilo"
"Mengine ni propaganda tu za kutengeneza taharuki kwa mashabiki wetu. Kwa 90% tayari wachezaji waliohitajika, wameshasaini mikataba na sasa bado kuwatambulisha tu"
"Tukimaliza kuzindua jezi wiki ijayo, Wananchi watafurahi vyuma vitakavyoshuka. Tunajua kuna watu wanaogopa ndio maana wanaanzisha propaganda"