KONDE GANG HAKUNA MSANII MWENYE GARI LAKE BINAFSI- CHEED
Aliyekuwa msanii wa Konde Music Worldwide, Cheed amedai kuwa hakuna msanii wa Lebo hiyo ambaye amewahi kuwa na gari lake kama inavyoonekana mtandaoni.
Utakunbuka Cheed aliachana na lebo hiyo mwaka jana pamoja na wasanii wenzake, Country Boy, Killy na Anjella.
"Hakuna msanii wa Konde Gang ambaye anamiliki gari, hicho ndicho kitu ambacho unatakiwa ukijue. Sio msanii, sio mfanyikazi, ukikuta gari pale ni la ofisi".
"Wewe utalitumia kwenda studio, kwenda mahojiano lakini hiyo ni mali ya kampuni,” amesema Cheed akiongea na East Africa Radio.
Kwa sasa Konde Music imesalia na msanii mmoja tu ambaye ni Ibraah, huyu pia ndiye alikuwa wa kwanza kusainiwa.