NYOTA SIMBA QUEENS AISHUTUMU POLISI

Mchezaji wa timu ya Wanawake ya Simba (Simba Queens), Jentrix Shikangwa raia wa Kenya ametupa lawama kwa jeshi la polisi nchini Kenya kwa kuzuia zawadi zake alizozipata katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Kupitia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Shikangwa ameandika "Nina furaha na huzuni sana kwa wakati mmoja mwezi huu nilipewa heshima ya kupokea tuzo ya kiatu cha dhahabu na kujumuishwa miongoni mwa wachezaji bora katika timu ya msimu katika msimu uliomalizika wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania lakini sikuweza kutwaa (kuchukua) tuzo zangu kwani nilikuwa nafanyia kazi baadhi ya mambo binafsi"

"Kwa hivyo kwa kuwa sikuweza kuchukua, tuzo zilitumwa kama kifurushi kupitia Tahmeed ambayo iliweza kufika (27/06/2023) karibu 12PM.

Kwa hivyo nilimwomba Shemeji yangu (Mume wa dada yangu) kwenda kuzichukua kwa niaba yangu ofisi za Tahmeed jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani, walimbeba wakampeleka kituo cha Polisi cha Kamukinji wakimuuliza alitoa wapi hivyo vitu"

"Polisi walinipigia simu kuthibitisha kama nimemtuma kuzichukua na ndiyo nilithibitisha lakini bado waliamua kumweka kizuizini, eti nalazimika ili aachiliwe"

Je, kuna kosa kumtuma mtu kukuchukulia zawadi?


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA