SIMBA KUISTAAFISHA JEZI NAMBA 20 YA MKUDE
Klabu yetu ya Simba SC imestaafisha jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa kiungo wetu Jonas Gerald Mkude ‘Nungunungu’ uamuzi ambao ni sehemu ya heshima ambayo viongozi wetu wameamua kumpa nyota huyo baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 13.
Mkude ambaye alitokea kwenye shule ya vijana ya Simba SC na kudumu katika kikosi cha wakubwa kwa takribani miaka 13 ameondoka klabuni Simba Sc baada ya mkataba wake kufikia ukomo.
Jezi namba 20 haitakuwepo msimu ujao hadi pale atakapopatikana mhitimu mwingine mwenye kuakisi kile ambacho Mkude amefanya klabuni hapo.
Aidha klabu yetu imepanga kumfanyia makubwa @jonasmkude20 ikiwa ni kumuaga kwa heshima siku ya Simba Day 2023, Inayotarajiwa kufanyika August 8,8,2023, huku ikimpa nafasi ya kurejea klabuni hapo baada ya maisha ya kucheza mpira kama ilivyo kwa Mussa Hassan Mgosi.